Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Mazingira Wezeshi kwa Wawekezaji wa Ndani na Nje ya Nchi ni Muhimu katika Ukuaji wa Uchumi


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeielekeza Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imeilekeza Wizara ya Uwekeazaji Viwanda na Biashsra kuhakikisha kuwa Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka, 2022 inayopendekezwa inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje wenye nia ya kuwekeza Tanza[1]nia ili kukuza uchumi wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Wajumbe wa Kamati hiyo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wake Mhe. Omary Mohamed Kigua wakati wa mafunzo kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania wa mwaka 2022 utakaofuta Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997, mafunzo hayliyofanyika kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti Oktoba 20, 2022 Bungeni jijini Dodoma.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji nchini na kuboresha utekelezaji na utendaji katika kushughulikia masuala ya wawekezaji ili kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini

Akijumuisha maoni na mapendekezo ya Wajumbe wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigae amesema Wizara itayafanyia kazi maoni na mapendekezo hayo yaliyotolewa ili kuhakikisha kuwa Sheria inayotungwa inaweka mazingira wezeshi yatakayovutia wawekezaji kuwekeza na kuendeleza biashara zao kwa maslahi ya Taifa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali akitoa mafunzo kwa Kamati hiyo amesema muswada huo umegawanyIka katika sehemu kuu tano ambazo zinahusu masharti mbalimbali ya uratibu na usimamizi wa masuala yote ya uwekezaji pamoja na  haki na wajibu wa Serikali na wawekezaji