Habari
MHE.KIGAHE: TANZANIA NA JAPAN KUENDELEZA USHIRIKIANO.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amesema Tanzania na Japan zitaendelea kushirikiana hasa katika miradi ya viwanda, barabara, na biashara ili kuendelea kupiga hatua katika nyanja za ajira, teknolojia ya kisasa, na kuimarisha biashara za nje.
Ameyasema hayo wakati wa kongamano la uwekezaji baina ya Tanzania na Japan lililofanyika leo Januari 14, 2025, Jijini Dar es Salaam .
Mhe.Kigahe amesema hatua hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa uwekezaji nchini, akibainisha kuwa Tanzania na Japan zina uhusiano wa muda mrefu katika sekta za maendeleo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Hisayuki Fujii, amepongeza uhusiano wa kidiplomasia na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, akisema mkutano huu umefungua milango ya uwekezaji mpya.
Katika Kongamano hilo kampuni mbalimbali zimekutana na kampuni 50 za Kitanzania na kubadilishana uzoefu na teknolojia pamoja na kujadili mambo mbalimbali ya ushirikiano wa kibiashara.