Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Michezo ni muhimu kwa afya na inaleta Motisha katika Utendaji kazi wa watumishi


 


Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema michezo ni muhimu kwa afya na inaleta motisha na hamasa kwa utendaji kazi wa watumishi.

Kigahe ameyasema hayo Oktoba 21, 2022 katika hafla fupi ya mapokezi ya  kombe la ushindi wa mchezo wa bao katika mashindano ya SHIMIWI yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara Mtumba, jijini Dodoma.

Aidha, Naibu Waziri Kigahe ameipongeza Timu ya Wizara iliyoshiriki mashindano hayo na  ameishauri Menejimenti ya Wizara kuanza kutenga fedha kwa ajili ya maandalizi ya michezo mbalimbali ikiwemo ununuzi wa vifaa ili kuiwezesha Wizara kuchukua makombe ya michezo mbalimbali katika michezo ya SHIMIWI ya mwaka ujao.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu akimkaribisha Naibu Waziri ameipongeza timu hiyo na kuahidi kuwa Wizara itabuni na kuandaa programu mbalimbali za michezo kama vile bonanza na michezo ya kirafiki ili kujiandaa na mashindano yajao, kuboresha afya za watumishi na kuongeza motisha kwa watumishi katika utendaji kazi

Vilevile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara - Viwanda na Biashara Dkt. Hashil  Abdallah  ameipongeza timu hiyo ya wizara kwa kufanya vizuri katika maeneo mengi ikiwemo timu ya mpira wa miguu iliyofanyikiwa kushinda mechi tatu (3) katika mechi (4) iliyopangiwa na kupata pointi (9) katika hatua za makundi  na kuishauri timu hiyo kuendelea na mazoezi mara kwa mara ili kujiandaa vyema katika mashindano yajayo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Bi. Veronica Nchango amesema timu ya wizara iliyoshiriki ni miongoni mwa timu 63 zenye jumla ya wanamichezo 2,510 wanaotoka katika Wizara 27, Mikoa 18 na Idara zinazojitegemea na wakala wa Serilkali 18 iliwezeshwa na wizara kwa kushirikiana na Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini.