Habari
DKT.JAFO ATAKA MWANANCHI APATE BIDHAA ZENYE UBORA
DKT.JAFO ATAKA MWANANCHI APATE BIDHAA ZENYE UBORA
Waziri wa Viwanda na BiasharaMhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) amewataka Wakala wa Vipimo (WMA) kuendelea kusimamia ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani lengo likiwa ni kuhakikisha mtumiaji wa mwisho anapata bidhaa zenye ubora.
Amebainisha hayo katika Kikao cha Menejimenti ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti katika kipindi cha bajeti ya 2024-2025 kilichofanyika leo Mei 13,2025,Jijini Dodoma.
Dkt.Jafo amesema atasimamia zaidi katika jambo la kutaka haki za watu kwa kuhakikisha haki watu zinapatikana na kuwapongeza WMA kuongeza nguvu zaidi kwa wale wanaokikuka sheria pamoja na kupongeza baadhi ya viwanda kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora.
Aidha Dkt. Jafo amewataka Mameneja hao watumie hekima badala ya kutumia nguvu na ubabe katika utendaji kazi wao kwa kuangalia pia na suala la utu hasa kwa wazalishaji wadogo ila kwa wale wazalishaji wakubwa ni lazima wafuate sheria.
Aidha Waziri Jafo amewaomba watendaji hao kuongeza upendo katika kazi zao kwa kuacha kutengenezeana matatizo katika kazi zao kwani lengo ni kuhakikisha kazi zinaenda vizuri kwani kwa kufanya hivyo watapata mafanikio makubwa.
Naye,Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Bw. Alban Kihulla,amesema katika utekelezaji wa bajeti ya 2024-2025 malengo yalikuwa ni kuhakiki vipimo ikiwemo mafuta yanayoingia nchini.
Vilevile Bw.Kihulla amesema kuna kanuni kuhusu rumbesa aliyoisaini na kuikataza na wao wameisimamia kwa vitendo kuhakikisha mkulima ananufaika na pia kwa sasa wazalishaji wa nondo wanazalisha nondo zenye ubora na unene ambao upo sahihi.