Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI JAFO AELEZEA MAFANIKIO MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA WAZIRI JAFO:VIWANDA VIMEONGEZEKA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA


WAZIRI JAFO AELEZEA MAFANIKIO MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

WAZIRI JAFO:VIWANDA VIMEONGEZEKA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) ametaja mafanikio iliyopata katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita ikiwemo kuongezeka kwa Viwanda ambavyo vimeongeza ajira kwa watanzania.

Hayo ameyasema Mei 15,2025 jijini Dodoma wakati akielezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Waziri Jafo amesema katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita, Viwanda vimekuwa vingi ambavyo vimetoa fursa ya ajira na kuongeza Pato la Taifa.

Ameongeza kuwa uwepo wa kiwanda cha Makaa ya Mawe kumeongeza ajira kwa watanzania na Serikali imefungua Bandari ya Mtwara kwa ajili ya kusafirisha makaa ya mawe.

"Mradi wa Katewaka utasaidia kupata ajira kwa vijana.Niwapongeze NDC kwa kusimamia hili.Baba wa Taifa wa Nchi yetu aliigawanya kwa kuwa na Viwanda vingi,Mwanza,Tanga,Morogoro na mwendelezo umekuwa ni mzuri,"amesema Waziri Jafo.

Uwepo wa Viwanda vya Sukari,mbolea na kuwa na eneo maalumu la Kwala ambalo kuna Viwanda vingi kumezidi kufungua fursa za ajira.

Amesema wamefanikiwa katika uzalishaji wa bidhaa muhimu ikiwemo uunganishaji wa vifaa vya magari na kuna Viwanda 15.

Amesema Viwanda hivyo uzalishaji wake ni mkubwa na ajira za wazawa ni nyingi kuliko wageni wanaotoka nje ya nchi.

"Ni mafanikio makubwa mno.Niwaombe watanzania tuwe wazalendo na hii ni kazi kubwa inayofanywa na Rais.

Kwenye Viwanda vya vioo,Waziri Jafo amesema kwa sasa Tanzania ina Viwanda vinne ambapo imani ya Serikali kwamba imeishajitosheleza.

"Imani yetu tutaungana pamoja tutumie mali zetu kwa kununua Viwanda,soko letu tunapeleka mpaka nje ya Bara la Afrika na haya ni Mapinduzi makubwa,"amesema Jafo.

Aidha, kwa sasa Tanzania ina Viwanda vitatu vya Marumaru ambavyo vimekuwa vikihakikisha mahitaji ya ndani yanajitosheleza.

"Nchi yetu imeanza kujitosheleza kwenye kila kitu ndio maana Nchi zingine zinaagiza,"amesema Waziri Jafo