Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WAZIRI KAPINGA ATATUA CHANGAMOTO ZINAZOKIKABILI KIWANDA CHA MARUMARU CHA GOODWILL


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb) akisikiliza na kutatua changamoto zilizowasilishwa na Uongozi wa Kiwanda cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani, Desemba 11, 2025.

Kiwanda cha Goodwill Ceramic kinazalisha milioni 14.4 za mita za mraba za marumaru kila mwaka na kinatoa ajira 1,600 za moja kwa moja

Kiwanda hiki pia kinapanua biashara yake katika bidhaa za majumbani na vyombo vya Usafi, na inakusudia kuanzisha kongani ya viwanda kubwa yenye thamani ya Dola za Marekani 1.5 bilioni ambayo inatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000.

Kongani hiyo itahusisha viwanda vyepesi na vizito, ikiwemo uzalishaji wa karatasi, mabati na kuchakata viazi vitamu na muhogo.

Waziri Kapinga alisema kuanzishwa kwa kongani hizi ni sehemu ya mkakati wa Serikali kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Katina kutoa ajira milioni Nane 8 na kuongeza mchango wa viwanda katika uchumi na Kurumiya malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.