Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe afungua mkutano wa majadiliano ya fursa za uwekezaji na wafanyabiashara wa kampuni 27 kutoka Nchini Ufaransa


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe afungua mkutano wa majadiliano ya fursa za uwekezaji na wafanyabiashara wa kampuni 27 kutoka Nchini Ufaransa ambapo amesema kuwa lengo la Mkutano huo na Wafanyabiashara hao ni kujadili namna ya kuwekeza nchini Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo Teknolojia za miundombinu, nishati, usafirishaji na Maendeleo ya miji.

Amebainisha hayo Mei 27,2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano huo na kuongeza kuwa mkutano huo ni muendelezo wa majadiliano yaliyofanywa na wafanyabiashara hao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan alipotembelea nchini humo Mei 2024.

Mhe.Kigahe amesema ziko fursa kubwa za masoko nchini Ufaransa kwa bidhaa za kahawa, samaki za aina mbalimbali na hata mbegu za mbogamboga na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa katika eneo hil kwa kuwa serikali iko tayari kukaribisha wawekezaji kutoka Ufaransa jambo litakalokuza uchumi wa Tanzania.

Amesema Kwa mujibu wa takwimu za Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Ufaransa imewekeza Tanzania katika miradi 41 ya kilimo, ujenzi, usafirishaji, huduma,taasisi ,a fedha pamoja na rasilimali watu yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 104.34 ambayo imetoa ajira 2379 Nchini.

Aidha ujumbe huo umesaini mikataba wa utunzaji wa mazingira pamoja na bayoanuai za misitu baina yao na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kupitia ujumbe huo wataona namna ya kushirikiana ili kuboresha kilimo katika kuongeza thamani katika mazao lakini pia kuongeza wigo wa kuuza bidhaa nchini Ufaransa.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hailaouit amesema Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye utawala Bora na kuwa na Mazingira Bora ya uwekezaji na amesema uwekezaji kwa wafaransa sio wa muda na kuondoka bali ni endelevu wenye tija na manufaa kwa nchi zote.

Nae Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe.Ali Mwadini amesema Tanzania ni mojawapo ya nchi yenye miundombinu imara na inayounganisha mipaka mbalimbali pia ina rasilimali zinazohitaji uendelevu kwa kizazi kijacho na serra nzuri za uwekezaji