Habari
Ni muhimu Kiwawezesha Wanawake na Vijana barani Afrika chini ya AfCFTA

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said amesema,mkutano wa Wanawake na Vijana barani Afrika chini ya AfCFTA umefanyika wakati mwafaka kwa kuangalia changamoto zinazowakabili wanawake na vijana lakini pia umewaleta vijana wenyewe katika mjadala.
Ameyasema hayo Septemba 14, 2022 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla za kifunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika ulioanza Septemba12 hadi 14, 2022.
"Hilo ni jambo muhimu sana mkutano huu umewaleta pamoja makundi ya vijana na wamekuwa wakijadili changamoto ambazo naamini baada ya mkutano huu Sekretarieti ya AfCFTA itayachukua maazimio, kwa kushirikiana na wawakilishi wa Serikali katika mkutano huu kwenda kuyafanyia kazi,"Amesema.
Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Mhe. Riziki Pembe amesema kuwa,wizara zote mbili zinaunga mkono juhudi zilizochukuliwa na Bara la Afrika katika kuwakomboa wanawake na vijana kiuchumi.
Amesema, hiyo ni sehemu ya kimkakati katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alisisitiza ili Taifa likuwe kiuchumi, kundi hilo lazima pawepo ushirikishwaji katika uundaji wa sera za uchumi na kutengewa bajeti katika suala zima la jinsia.
Amesema pia ni muhimu kusaidia ushiriki wa biashara ndogo za kati na kubwa kwa wanawake na vijana ili kuhakikisha mafanikio makubwa yanapatikana miongoni mwa kundi hilo na Taifa kwa ujumla.
"Kwa hiyo, no wajubu wetu kuona kwamba wanawake na vijana wanashiriki katika maendeleo katika bara letu la Afrika na kuyafikia masoko, kitaifa, kikanda na Kimataifa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika majadiliano ya kibiashara" Bi Pembe