Habari
Ongezeni Nguvu ya Kuwezesha Wananchi Kiuchumi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wadau wote wa uwezeshaji wananchi kiuchumi waongeze nguvu katika kutoa huduma za uwezeshaji hasa maeneo ya pembezoni ya miji na vijijini ili kufikia malengo ya nchi katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Ametoa wito huo Septemba 19, 2022 wakati akifungua kongamano la sita la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, lililofanyika katika ukumbi wa PSSSF, Jijini Dodoma.
“Pamoja na wito huo, Mikoa ambayo imeanzisha vituo vya uwezeshaji iendelee kuboresha miundombinu ili vituo hivyo vikidhi ubora na viwango katika kutoa huduma za uwezeshaji”
Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani Serikali imeendeleza azma yake ya kuwawezesha wananchi ambapo katika mwaka 2021/22, Serikali kupitia mifuko na programu mbalimbali
Imeweza kutoa mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya shilingi bilioni 903 kwa wanufaika wapatao milioni 5.9 nchi nzima”.
Ameongeza kuwa katika mwaka 2021/2022 jumla ya watanzania 72,395 walipata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kutokana na ushiriki wao kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji (Local Content). “Aidha, miradi ya kimkakati ilitoa kandarasi ndogo kwa kuingia mikataba na kampuni 2,019 za Watanzania kwa huduma mbalimbali