Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

ZAIDI YA SH. BILIONI 28 KUJENGA KITUO CHA UPANDIKIZAJI FIGO TANZANIA*


ZAIDI YA SH. BILIONI 28 KUJENGA KITUO CHA UPANDIKIZAJI FIGO TANZANIA*

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo pamoja na utoaji mafunzo kwa madaktari bingwa ambacho kitakuwa ni kikubwa katika ukanda wa Jangwa la Sahara.

Kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ni ushirikiano kati ya Shirika la Tiba la TOKUSHUKAI, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma na kinatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 28 ikiwa ni msaada usiokuwa na masharti yoyote.

Utiaji saini huo umefanyika Mei 26, 2025 wakati kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025. Kongamano hilo lilifunguliwa na Mheshimiwa Majaliwa.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Profesa Abel Makubi amesema wamesaini makubaliano na shirika hilo linaloundwa na kundi la madaktari Wakijapan ambao wamekuwa wakisaidia utoaji na uboreshaji huduma za afya.

Amesema mbali na ujenzi wa kwa ajili ya kujenga kituo cha umahiri katika upandikizaji figo kwenye eneo la Tanzania na Ukanda wa Jangwa la Sahara ambacho kitajengwa ndani ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na kutarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma ndani ya miaka mitatu kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania

Profesa Makubi amesema pia kituo hicho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa ajili ya kupandikiza figo, pamoja na kufanya tafiti kwa ajili ya kuzuia au kupunguza magonjwa yanayohusiana na figo kwa ushirikiano kati ya Hospitali hiyo na UDOM.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Lugano Kusiluka amesema makubaliano hayo yataimarisha huduma ya upandikizaji figo ambao unafanyika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ushirikiano wa wataalamu wa hospitali hiyo pamoja na wa UDOM.