Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

PROF. GODIUS KAHYARARA AWASILISHA TAARIFA YA HALI YA UWEKEZAJI NCHINI KWA KAMATI YA BUNGE.


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uwekezaji nchini Kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Katiba na Sheria Leo tar. 7 Februari, 2022 Bungeni jijini DODOMA.

Katika taarifa yake Prof. Kahyarara ameieleza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuwa katika kipindi Cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita, thamani ya Uwekezaji imeongezeka Kwa kiasi kikubwa kufikia USD bilioni 4 ambapo hiyo imechangiwa na juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini.

Prof. Kahyarara amesema kupitia Blue print changamoto Kwa wawekezaji zinaenda kupunguzwa Kwa kiasi kikubwa ambapo hatua ya uanzishwaji wa One Stop Centre unaenda kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji.