Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Prof. Kahyarara asisitiza sekta binafsi kutumia fursa za biashara katika Kongamano la Jumuiya ya Madola 2022 Kigali, Rwanda.


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara akizungumza Kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amewahimiza wajumbe wa CEOrt kutumia fursa za Biashara na kuchochea maslahi ya umma katika kongamano lijalo la Biashara la jumuiya ya Madola 2022 linalotarajiwa kufanyika tar. 21 - 23 Juni, 2022 Kigali nchini Rwanda.

Prof. Kahyarara Amesema kuwa jukwaa hili lililoandaliwa na ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania na CEOrt wenye lengo la kuhamasisha sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kongamano la Biashara la Jumuiya ya Madola 2022.

Kwa mwaka huu 2022 kongamano hili litafanyika nchini Rwanda na kuufanya mkutano huo kuwa wa kwanza na mkubwa zaidi wa ana kwa ana Kwa Serikali na Biashara katika Jumuiya ya Madola tangu kuanza kwa janga la Uviko 19.

Naye mwenyekiti wa Jukwaa la CEOrt Bw. Sanjay Rughani ameipongeza Serikali ya awamu ya sita Kwa Ushirikiano wanaoutoa Kwa sekta binafsi katika kukuza uchumi.

Bw. Rughani amesema kuwa jukwaa la CEOrt linawakilisha wakurugenzi watendaji kutoka Kampuni zaidi ya 170 nchini Tanzania katika sekta mbalimbali Kwa lengo la kuchochea uongozi wenye kujenga ustawi endelevu wa kijamii na kiuchumi kupitia ajira, kodi, teknolojia na kukuza ujuzi.

Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar na balozi wa Rwanda nchini Tanzania.