Habari
MATOKEO YA ZIARA YA WAZIRI KAPINGA NCHINI CHINA YAENDELEA KUONEKANA
Kufuatia ziara ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb), nchini China mwezi Machi 2026 kwa ajili ya kutafuta na kuvutia wawekezaji wa kimkakati katika sekta ya viwanda, Tanzania imeendelea kuona matokeo chanya ambapo wawekezaji kutoka China wamefika nchini kwa lengo la kuwekeza katika sekta mbalimbali za uzalishaji.
Wawekezaji hao kutoka Jimbo la Guangzhou, wakiwakilisha kampuni ya Guangzhou Songsheng Enterprise Management Company Limited, wamefanya kikao na Mhe. Kapinga kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji nchini. Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Bodi, Bw. Hao Liao; Mkurugenzi Mwendeshaji, Bw. Leon Liao pamoja na Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Cruld Liao.
Kikao hicho kilikuwa na mafanikio makubwa, kikilenga kujadili fursa za uwekezaji wa viwanda, kuongeza biashara kati ya Tanzania na China, uhamishaji wa teknolojia, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
Hatua hizi ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kukuza uwekezaji, kuongeza thamani ya rasilimali za ndani, kujenga uwezo wa uzalishaji wa ndani, na kuunga mkono azma ya Tanzania ya kujenga uchumi shindani wa viwanda kuelekea kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050.
