Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Sekta binafsi inajukumu muhimu katika maendeleo ya Tanzania, ikichangia katika kuongeza ajira, uvumbuzi, Pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.


Serikali imesisitiza kuwa sekta binafsi inajukumu muhimu katika maendeleo ya Tanzania, ikichangia katika kuongeza ajira, uvumbuzi, Pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Vilevile Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia uwekezaji nchini hususani katika kukuza mazingira thabiti yanayowezesha Watanzania kuonyesha vipaji vyao, kama ilivyothibitishwa na Impact Business Breakfast (IBB), yenye jukumu muhimu katika maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, wakati wa Hafla ya Tuzo za Biashara za Impact za 2024.

Aidha, alibainisha kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono matukio kama IBB, kwani ni muhimu kwa kupata maarifa mapyayanayohitajika kuendeleza uchumi wa nchi.

Aliongeza, “Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali inatambua umuhimu wa ubunifu kutoka kwa wataalamu wetu na itaendelea kuunga mkono wabunifu.”

Dkt. Abdallah alisisitiza kuwa IBB ni jukwaa linalowaleta pamoja makundi matatu muhimu ya wataalamu kwa lengo la kiwahamasisha na kuwawezesha kubadilisha uzoefu: Kundi A (usimamizi wa juu), B (usimamizi wa kati), na Kundi C (vijana wataalamu), wakiongoza katika sekta mbalimbali.

Vilevile ameongeza kuwa jukwaa hilo linaandaa mikutano ya mara mbili kwa mwezi inayowapa wafanyabiashara maarifa muhimu kuhusu kanuni za biashara zilizo thibitishwa ili kuimarisha uwezo wao wa usimamizi wa biashara na utendaji kazi.

Aliongeza kuwa mbinu ya kipekee ya IBB inaleta wataalamu kutoka sekta mbalimbali pamoja kubadilishana uzoefu, maarifa, na mbinu bora za maendeleo ya biashara.

“Tukio hili limekuwa tukio la kitaifa ambalo limeimarisha ushirikiano katika sekta nyingi,” aliongeza, Mbali na IBB, Impact Advisory inatoa uongozi na suluhisho maalum kwa usimamizi wa miradi ya kimaendeleo na biashara endelevu,” alisema Dkt. Abdallah.

Dkt. Abdallah alieleza kuwa Mada ya Tuzo za Biashara za Impact 2024 ni “Jukumu la Sekta Binafsi katika Kufikia Ajenda ya Maendeleo ya Kitaifa ya Tanzania.”