Habari
Sera na Sheria za Viwanda na Biashara kufanyiwa maboresho

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Kilimo na Mifugo imeielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kufanya Maboresho ya Sheria na Sera za Viwanda na Biashara ili kuboresha mazingira mazuri kwa wafanyabiashara.
Hayo yamesemwa Oktoba 18, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati Mhe Deodatus Mwanyika (Mb) wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya Utekelezaji wa Taasisi za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Wakala wa Vipimo(WMA)
Aidha amezitaka Taasisi hizo kutoa Elimu yakutosha kwa umma kuhusu Leseni za Biashara na Vipimo mbalimbali vya bidhaa nchini.
Vilevile ameipongeza Taasisi ya BRELA kwa uendeshwaji wake na ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuitaka taasisi hiyo iongeze kasi ya kukusanya mapato kwakua na wigo mkubwa wa wafanyabiashara
Nao Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kutoa maoni mbalimbali kuhusu mfumo wa leseni, vifungashio(ujazo wa rumbesa) katika bidhaa mbali mbali, vipimo vya mita za maji, mita za umeme na usimamizi wa sheria na Sera katika taasisi hizo
Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) akijumuisha maoni na mapendekezo yaliotolewa na kamati amesema Serikali ipo tayari kupitia nakufanya marekebisho ya sera na sheria za viwanda na biashara ili kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara.
Aidha amesema serikali ipo katika majadiliano ya kufanikisha Leseni moja kwa wafanyabiashara ili kuweza kujua kazi na uwajibikaji katika kila kampuni ili kuongeza ufanisi katika uwajibikaji