Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI imeshaanza mchakato wa kupanga eneo la ekari 639 ambalo litapangwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda


SERIKALI imeshaanza mchakato wa kupanga eneo la ekari 639 ambalo litapangwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na biashara na tayari mshauri ameshapatikana.

Haya yabainishwa bungeni na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) wakati wa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe.

Akiuliza swali la nyongeza, Mafuwe alisema: “pamoja na mpango huo mzuri wa kujenga viwanda na miundombinu mingine kutokana na adha kubwa inayowakabiri wananchi wa ukanda wa Machame kuenda kufuata bidhaa Moshi mijini au maeneo mengine.”

Hivyo alitaka kujua kama Serikali haioni ipo haja sasa ya kuweka mji mdogo wa kibiashara ambao bidhaa na vitu vingine vitapatikana njia panda ya Machame

Pia alitaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa kiwanda cha Losa ili kianze kutoa huduma

Akijibu swa hilo, Kigahe alisema

Akijibu swali hilo, Kigahe alisema Serikali imeshamapata mshauri ambaye atashauri namna ya kupanga eneo hilo ili kuwe na meneo ya makzi na husuka za kijamii na maeneo ya biahsara katika Mji mdogo wa Machame kuwezesha wananchi kufanya biashara.

Alisema pia Serikali kupitia Shirika la Kuendeleza Kiwanda Vidogo (SIDO) imepanga bajeti ya kufufua kiwanda cha Losa ili wananchi wanufaike na uwepo wa kiwanda hicho.

Katika swali la msingi Mafuwe alitaka kujua ni lini Serikali itakamilisha ahadi yake ya kutenga maeneo maalum ya Biashara kwenye eneo la NDC Kiwanda cha KMTC njia panda ya Machame.

Akijibu swali hilo, Kugahe amesema mpango Mkakati wa matumizi ya eneo la KMTC chini ya NDC ilikuwa ni kujengwa viwanda mbalimbali, makazi ya wafanyakazi wa Viwanda na mahitaji mengine.

Amesema kwa sasa, kimejengwa Kiwanda cha Kuzalisha Mashine na Vipuri cha KMTC kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 16.

Kigahe amesema eneo lenye ukubwa wa jumla ya ekari 639 linaandaliwa mpango wa Uwekezaji kwa ajili ya kujenga Mji wa Viwanda (SMART INDUSTRIAL CITY).

Amesema mpango huo umewekwa katika Vipaumbele vya Mwaka wa Fedha 2025/2026 vya Sekta ya Viwanda na Biashara ambao utahusisha ujenzi wa miundombinu ya msingi ikiwemo barabara, mifumo ya maji safi na maji taka, umeme na Industrial sheds.