Habari
TANZANIA NA SINGAPORE KUIMARISHA USHIRIKIANO WA BIASHARA
Tanzania na Singapore zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa Biashara na viwanda kwa kulenga uendelezaji wa viwanda vidogo na biashara ndogo, kwa kutumia fursa za Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuimarisha mnyororo wa thamani kwa wajasiriamali kuwezesha bidhaa za Tanzania kushindana katika masoko ya kimataifa.
Makubaliano hayo yamefikiwa Aprili 27, 2026, jijini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu, Bw. Aristides Mbwasi, alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Biashara ya Asia, Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda ya Singapore, Bw. Adrian Ng, katika Ofisi za Wizara Mtumba. Mazungumzo hayo yanadhihirisha azma ya dhati ya kuimarisha diplomasia ya kiuchumi na kufungua fursa mpya za Biashara na uwekezaji kati ya mataifa haya mawili.
