Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

TANZANIA NA SLOVAKIA KUIMARISHA UHUSIANO WA BIASHARA VIWANDA NA UWEKEZAJI


Tanzania na Slovakia zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa biashara, viwanda na uwekezaji kwa kupitia mikutano ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Slovakia (B2B).

Makubaliano hayo yamefanyika wakati wa mazungumzo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb) alipokutana na Balozi wa Slovakia nchini Mhe. Ivan Lančarič Aprili 27, 2026 katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma

Aidha, Viongozi hao pia wamejadiliana na kukubaliana kuhusu kuendeleza ushirikiano katika uanzishaji na uendelezaji wa Viwanda vya kutengeneza magari, Mitambo mbalimbali na kukuza biashara kwa ujumla baina ya Nchi hizo ambapo Tanzania iko tayari kwa uwekezaji huo.