Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inaendelea kutatua changamoto zilizopo katika viwanda vya Katani


Waziri wa  Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt .Ashatu Kijaji  (Mb.) amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili viwanda vya kuchakata katani ili kuliendeleza zao hilo la kimkakati katika kukuza biashara, kuongeza ajira na kuongeza pato la taifa.

Waziri Kijaji ameasema hayo alipokuwa akiongea na  wafanyakazia  wa Kiwanda cha 21st Century Holdings LTD kinachojihusisha na uchakataji wa  kamba zinazotokana na mkonge kilichopo chang'ombe jijini Dar es salaam,   mara baada ya kufanya  ziara katika kiwana hicho Juni 17, 2022

Akiongea na wafanya kazi hao Dkt. Kijaji amesema katika kutatua changamoto hizo Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mazao yote yanayotokana na zao Mkonge  ikiwa ni lalamiko lao kubwa la wenye viwanda vinavyozalisha bidhaa za katani.

Pia amesema Serikali inaendelea kushughulikia changamoto nyingine uli kuviwezesha viwanda hivyo kushiriki kikamilifu katika soko la ushindani ndani ya nchi kikanda na kimataifa 

Aidha  amewahakikishia wafanyakzi wa kiwanda hicho kuwa  kiwanda hicho hakitafungwa kwa kuwa Serikali inashughulikia changamoto zinazokikabili kiwanda hicho pamoja na zinazowakabili wafanyakazi hao  ikiwemo upatikanaji wa haki zao za msingi iwapo kiwanda hicho kitafungwa kwa kufuata sherua na taratibu zilizopo