Habari
Serikali inaendelea na hatua mbalimbali kutatua changamoto zote zinazovikabili Viwanda vya Sukari nchini

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Upande wa Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mei 26, 2022 ameihakikishia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda Biashara na Mazingira kuwa changamoto zote zinazokikabili.kiwanda cha Sukari cha kagera katika upanuzi wa uzalishaji wa sukari zitatatuliwa ili kukiwezesha kiwanda hicho kuzalisha tani 150000 kwa mwaka na kuchangia kuondoa upungufu wa Sukari uliopo nchini.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira imefanya ziara ya mafunzo katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kuangalia uzalishaji wa sukari na mikakati iliyopo ya kuongeza uzalishaji wa sukari ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza nje ya nchi