Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali inaendelea na Mpango wa Kuratibu Uwekezaji wa Viwanda vya mbolea nchini.


Serikali inaendelea na Mpango wa Kuratibu Uwekezaji wa Viwanda vya mbolea nchini.

Haya yamebainishwa bungeni jana na Naibu Waziri, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Mhe.  Exaud Kigahe ( Mb.)  wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Tabora Kaskazini Athuman Maige(CCM).

 Katika swali lake, Maige alitaka kujua mpango wa Serikali wa kujenga Viwanda vya Mbolea nchini ili Wakulima waongeze tija.

 Akijibu swali hilo, Kigahe alisema Serikali inaendelea na Mpango wa Kuratibu Uwekezaji wa Viwanda vya mbolea nchini.

“ Matokeo ya Uratibu huo ni pamoja na kiwanda cha mbolea cha Minjingu na ujenzi unaoendelea wa kiwanda cha mbolea cha Itracom Fertilizer Limited, Jijini Dodoma.”