Habari
Serikali yatoa bilioni 14.4 Mradi wa Engaruka.

Serikali yatoa bilioni 14.4 Mradi wa Engaruka.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb) amefanya mkutano wa hadhara Januari 10, 2025 katika tarafa ya Mtowambu wilayani Monduli.
Lengo la mkutano ni kuwafahamisha wananchi kuwa Serikali imetoa shilingi bilioni 14.4 kwaajili ya utelelezaji wa mradi wa magadi soda wa Engaruka na ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo.
Aidha, wananchi 595 kutoka vijiji vinne vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni watanufaika na fidia ya shilingi bilioni 6.2 huku fedha zingine zilizobaki zikienda katika shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Dkt. Jafo alisema fedha hizo zimetolewa na Serikali ikiwa ni mkakati wa kuendeleza miradi ya kimkakati yenye tija kwa Taifa.
Ameongeza kuwa, awali mradi huo ulikwama kutokana na changamoto za kimazingira katika Ziwa Natroni na kupelekea kuchelewesha mradi huo lakini Serikali ikafanya utafiti tena na kuja na maamuzi kutoka kwa wataalam na kuona eneo la vijiji vinne linafaa sana katika uchimbaji magadi hayo ambalo ni eneo la uwanda wa juu wa ziwa hilo lenye magadi soda ya kutosha.
"Mradi huu wa magadi soda unaenda kuanza na mmepewa fidia hii kwaaajili ya kuanza mradi wake na shilingi bilioni 6.2 zinalipwa ili mradi uanze na sasa hivi zabuni zimeshatangazwa na tayari wawekezaji wameanza kuonesha nia ya kuwekeza kwenye mradi huu".
Viwanda vingi hapa Tanzania vinatumia magadi soda hayo na Tanzania ni waagizaji wakubwa wa magadi soda kutoka nchi za Boswana na maeneo mengine huku ikitumia fedha nyingi za kigeni kuagiza.
Hivyo mradi huo unaenda kuhamisha fedha hizo badala ya kununua nje magadi hayo yatatokea eneo la Engaruka
Dkt.Jafo amewashauri wananchi kuanza kufikiria kujenga hoteli na nyumba bora ili ziwe fursa kubwa zenye tija ikiwemo uchomaji nyama bora ili wawekezaji waje kula nyama na kula vyakula vinavyouzwa na wenteji wa maeneo haya.
Fedha zimeshaingizwa kwaaajili ya ulipaji fidia kupitia akaunti ya NDC huku fedha nyingine zitatumika kuendeshea mradi huo.
Naye Naibu Waziri wa Madini, Mhe.Dkt.Stephen Kiruswa alisema mradi huo uwe ni chimbuko la mafanikio kwa wananchi wa wilaya ya Monduli na Longido kwani mradi huu ni mkubwa