Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali Yawahakikishia Wajasiliamali na Wafanyabiashara Kuwawezesha Kiuchumi


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itahakikisha bajeti inayotengwa na kuelekezwa katika Halmashauri  kuwawezesha    Wafanyabiashara na Wajasrimali inawafikia moja kwa moja ili ikawasaidia kuinua kiuchumi na kuchangia  pato la Taifa kuongezeka.

Hayo yamesemwa na  Katibu Mkuu Kiongozi  wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said ikiwa ni mwendelezo wa siku ya pili ya Kongamano la Wanawake na Vijana katika biashara chini ya Eneo huru la Biashara Afrika linalofanyika kuanzia Swptemba 12 hadi 14 , 2022 JNICC Dar es Salaam 

Vilevile amesema kwa Upande wa  Zanzibar tayari zimetengwa fedha na kuwekwa katika benki ya CRDB ambayo inamuwezesha mwananchi kuchukua Mkopo pasipokuwa na riba wala kuweka dhamana kwani hapo awali wengi walikuwa wanakosa mikopo hiyo kwa kushindwa kupata vigezo hivyo vya dhamana 

"Serikali ya Zanzibari iliona adha ya wananchi wake kukosa mikopo hivyo Serikali imepunguza ule mzigo uliokuwepo wa riba kubwa na kuweka dhamana ili mtu apate mkopo  na sasa kila mtu ananufaika na fursa hiyo uaminifu wa kirudisha na wengine wapate.

Sanjari na hayo amesema kwa Tanzania bara kulikuwepo na  sheria mahusi na inayoziielekeza halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 Ili wananchi wakope wakajiendeleze katika shughuli zao za kiuchumi.

Aidha  amesema kongamano hilo limekuwa chachu ya kubadilishana uzoefu, kujenga uhusiano wa kibiashara na  kutatua changamoto za biashara hasa maeneo ya mipakani wanazokumbana nazo Wafanyabiashara .