Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Serikali yawakutanisha wazalishaji wa malighafi zinazotumika kutengeneza vitakasa mikono (hand sanitizer) Jijini Dodoma.


SERIKALI YAWAKUTANISHA WAZALISHAJI WA MALIGHAFI ZINAZOTUMIKA KUTENGENEZA VITAKASA MIKONO (HAND SANITIZER) LEO TAREHE 25 MACHI, 2020 UKUMBI WA LAPF DODOMA. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amefanya kikao na wamiliki na wasimamizi wa Viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono ( Hand Sanitizer). Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana na wenye viwanda, wazalishaji pamoja na wadau wengine watakavyoweza kuongeza uzalishaji ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa kwa ajiri ya kujikinga na usambaaji wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID19). Katika kikao hicho Kampuni la Kilombero Sugar imetoa lita 30,000 za alcohol bure kwa serikali zitaakazosaidia kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer) ili kusaidia juhudi za serikali za kupambana na virusi vinavyosababisha ugojwa wa Corona. Pia kampuni ya Consumer Choice Ltd imetoa kwa serikali kiasi cha lita 10,000 za ethanol na pia imeamua kubadili matumizi ya Ethanol ambayo yalipaswa kutengeneza vilevi ambapo asilimia 75% za Ethanol zitatengeneza vitakasa mikono (hand sanitizer) na 25% ya Ethanol itakayobaki itatumika kutengeneza vilevi. Kampuni ya Mount Meru Millers imetoa lita 10,000 ya Vitakasa mikono (Hand sanitizer) itakayosambazwa kwa vituo vya afya na taasisi nchini. Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amewataka wenye viwanda kuongeza uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vitakasa mikono pia amewaelekeza TBS na FCC kuendelea kukagua wafanyabiashara wa vitakasa mikono ambao wanauza bidhaa feki na hafifu pia kwa wote wanaopandisha bei kwa lengo la kujinufaisha kuwachukulia hatua kali za kisheria kwani wanahatarisha maisha ya watanzania.