Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Sheria ya Madini kwa Viwanda vya Saruji na Mbolea kurekebishwa


Sheria ya Madini kwa viwanda vya Saruji na mbolea kuboreshwa

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda  na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema kuwa Serikali  inafanya marekebisho ya Sheria ya Madini Sura ya 123, kifungu Na. 10(1). Iliyokuwa inavitaka Viwanda vya Saruji na mbolea kutoa asilimia 16 ya hisa huru (free carried interest – FCI) kwa Serikali.

Ameyasema hayo Februari 13, 2023 wakati wa kikao cha pamoja na Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) kilichofanyika 13/02/2023 jijini Dar es salaam kilicholenga kujadili changamoto zinazowakabili wenye viwanda ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa maboresho hayo yakikamilika  viwanda vya saruji na mbolea havitatambulika kama kampuni za uchimbaji madini ambazo zinatakiwa kutoa hisa hizo huru 16%. Vile vile ameongeza kuwa Serikali inaendelea kushighulikia kero nyingine ili kuifanya sekta binafsi inayoajiri watu wengi kufanikiwa

Aidha, Dkt. Kijaji amewashauri wamiliki wa viwanda nchini kizalisha kwa wingi bidhaa zenye ubora na viwango vinavyotakiwa katika soko la kimataifa ili kiweka kuingia katika soko la enwo huru la biashara  Afrika kwa ushindani na kitimiza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ya kuifanya Tanzania kuilisha Afrika na Dunia kwa bidhaa bora Inazokidhi mahitaji ya soko.

Naye Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba   amesema Serikali inaendelea  kutatua changamoto mbalimbali za kikodi  ikiwemo VAT na  ETS  na amewataka wamiliki hao wa viwanda kuwasilisha changamoto zao kwa barua Ifanyiwe  kazi ili kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia  wawekezaji nchini.

Kwa upande wa  CTI, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Bwana Leodeger Tenga amesema changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili wamiliki hao wa viwanda zimefanyiwa kazi na ameiomba Serikali  kufanyia kazi haraka changamoto zilizosalia ili kuvutia uwekezaji kwa wingi kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha, amewataka wamiliki wa  viwanda nchini kuzalisha bidhaa bora na zenye unafuu ili ziweze kuvutia masoko mengi na makubwa kwa Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.