Habari
Tani 337.7 ya asali imeuzwa masoko la nje
Tani 337.7 ya asali imeuzwa masoko la nje
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amesema kampuni ndogo 46 zinazozalisha asali zimeuza tani 337.3 katika masoko ya nje.
Kigahe ameyesema hayo bungeni wakati wa kujibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum Aziza Ally (CCM) swali lilioulizwa kwa niaba na Mbunge wa Jimbo la Tabora Kasikazini, Almas Maige.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Aziza Sleyum Ally (CCM), alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kutafuta soko la asali.
Akijibu swali hilo Kigahe amesema Serikali imekuwa na mkakati wa kutafuta soko la asali ambao unajumuisha mafunzo ya uzalishaji bora katika mnyororo wa thamani wa asali.
Pia ujenzi wa viwanda vya pamoja (Common Facilities) vya uchakataji bora wa asali, utangazaji wa bidhaa za asali zinazozalishwa nchini katika maonesho ya ndani, Kikanda na kimataifa.
Amesema pia kujumuisha fursa ya asali ya Tanzania katika majadiliano ya nchi na nchi, kikanda na kimataifa.
Kigahe amesema hatua hizo zimewezesha Kampuni ndogo 46 zinazozalisha asali kuuza tani 337.3 katika masoko ya nje, hususani soko la Ulaya ambapo nchi zinazonunua kwa wingi ni Ujerumani, Uholanzi na Poland na kufuatiwa na Soko la Afrika Mashariki katika nchi za Kenya, Rwanda na Uganda.
Alisema katika soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeuzwa katika nchi ya Botswana.
“Jumla ya mauzo katika masoko hayo kwa mwaka 2023 yalikuwa na thamani ya shilingi bilioni 2.”
Katika swali la nyongeza Maige alitaka kujua
Swali la nyongeza Maige alitaka kujua mpango wa Serikali wa kuanzisha shamba la nyuki la mfano kwa ajili ya ufugaji wa nyuki.
Pia alitaka kujua mpango wa Serikali wa kurahisisha upatikanaji wa zana kwa ufugaji nyuki ikiwa ni pamoja na mizinga na nguo za walina asali.
Akijibu maswali hayo, Kigahe alisema Serikali imekuwa ikiwasaidia wafugaji nyuki ili wazalishe kwa tija na kuwa wamekuwa wakitumia misitu ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kama maeneo ya kufugjia na kujifunza ufugaji.
Pia alisema taasisi mbalimbali zimekuwa zikitoa mizinga ya kisasa kwa wafugaji wa nyuki ili wafuge kisasa.