Habari
TanTrade Yatagaza Tarehe na Taarifa za Maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade, Latifa Khamis, amesema kuwa maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, yatafanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2025 katika viwanja vya Julius Nyerere ,Dar es Salaam.
Amebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa Maonesho hayo katika ukumbi wa CBE jijini Dodoma Mei 13,2025.
Bi. Latifa amesema katika kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yenye kaulimbiu isemayo: “Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.” yanafanyika kwa mafanikio, TanTrade imeandaa mikakati kadhaa ikiwemo, ukarabati wa majengo na miundombinu katika viwanja vya maonesho, ujenzi wa maeneo ya wazi kwa viwango vya kimataifa, kuimarisha usafi na huduma za afya, kuongeza idadi ya washiriki na wageni kwa kuandaa burudani mbalimbali.
Aidha ameeleza kuwa lengo la maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kukutana, kubadilishana uzoefu, kutafuta masoko pamoja na kujifunza teknolojia mpya. Aidha, maonesho haya yamekuwa pia sehemu ya kujifunza kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini.
Kwa upande wa wageni wa kimataifa, mabanda maalum yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza mapato ya fedha za kigeni. Mabanda hayo ni pamoja na, banda la Jakaya Kikwete, banda la Benjamin Mkapa, banda la Ally Hassan Mwinyi
Maonesho hayo yataambatana na matukio mbalimbali muhimu, yakiwemo,Juni 26, 2025 Mapokezi ya washiriki wa ndani,Juni 27, Mapokezi ya washiriki wa nje ya nchi, Julai 3, Uzinduzi wa programu ya Urithi Wetu, ikiwalenga wanafunzi kutoka vijijini wa mikoa mitano Pwani, Mbeya, Kigoma, Zanzibar Kaskazini na Kusini, Julai 5,Made in Tanzania Day siku ya kuenzi bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, Julai 8, Zanzibar Day, Julai 9, Siku ya Kimataifa ambapo Urusi inatarajiwa kushiriki, Julai 10, Hariana Day