Habari
Tanzania na Malawi zimekubaliana kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuendelea kushirikiana Kibiashara.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Tanzania na Malawi zimekubaliana kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuendelea kushirikiana Kibiashara.
Dkt. Jafo ameyasema hayo Mei 2, 2025 baada Nchi hizo mbili kutia saini Tamko la Pamoja (Joint Communiqué) kufuatia kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje; Kilimo;
Viwanda na Biashara wa pande zote jijiniDodoma.
Kusainiwa kwa Tamko la Pamoja ni uthibitisho wa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Malawi kwa bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo kulingana Mikataba na miongozo ya Kikanda na Kimataifa iliyopo.