Habari
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA UFUTA NA KARANGA NCHINI UTURUKI

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Sempeho Manongi ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mwaka wa mazao ya Ufuta na Karanga World Sesame & Peanut Conference (WSPC) unaofanyika Instanbul Uturuki.
Mkutano huo utafanyika ndani ya siku tatu, Septemba 5-7, 2025 ukiwa na lengo la kukutana na wanunuzi wa kubwa Duniani ili kupata soko la uhakika, kubaini teknolojia muhimu zinazoweza kurahisisha uzalishaji na kuongeza ubora kwa kujifunza kutoka kwa wadau na wazalishaji wakubwa kutoka nchi nyingine.
Mkutano huo wa siku tatu unawaleta Pamoja wadau wakuu wa Mazao ya Ufuta na Karanga duniani kuanzia Wakulima, Wasindikaji, Wafanyabiashara na Watafiti wa soko.
Katika Mkutano huo Tanzania inawakilishwa na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na sekta binafsi.