Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Kongamano la Biashara kati yake na Nchi za Umoja wa Ulaya


Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Kongamano la Biashara kati yake na Nchi za Umoja wa Ulaya litakalofanyika   Februari 23  - 24, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNlCC), Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika 17/02/2023, Dar es salaam, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji  akiwa ameambatana na Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Emilio Rossetti na ujumbe wake  pamoja na Mwakilishi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) Bi. Kinanasy Seif

Amesema Kongamano  hilo linalenga kuwaunganisha washiriki zaidi ya wafanyabiashara 600 kutoka katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ili kuwawezesha kubadilishana uzoefu, kushirikiana na watoa maamuzi na kukutana na wawekezaji wanaofaa pamoja na kujenga uelewa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo kwa sekta ya umma na binafsi ambapo, hati za makubaliano mbalimbali ya Uwekezaji baina ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya zitatiwa saini.

Aidha, Dkt. Kijaji amesema  Kongamano litazinduliwa  rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Samia Suluhu Hassan,

na litafungwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi ambaye atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha na hati za makubaliano.

Vilevile, Waziri amesema litahudhuriwa na Mawaziri nane (8) kutoka Serikali ya JMT na SMZ pamoja na Mabalozi sita (6) wa Tanzania katika nchi za Umoja wa Ulaya  ambao watashiriki katika vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Biashara, Serikali na Taasisi za Kifedha,

"Ninatarajia kuona kongamano hili la Biashara la kwanza kuwa fursa ya kuvutia wawekezaji, teknolojia na utalaamu katika nchi yetu na kuvutia biashara na uwekezaji kutoka duniani kote katika sekta za nishati, madini na kilimo endelevu." hivyo tunatarajia hati za makubaliano zitakazotiwa saini zitaendeleza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, zitaongeza ajira kwa vijana na zitachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu, Amesema Dkt. Kijaji.

Aidha, Dkt. Kijaji amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania kutumia fursa hiyo vizuri kuendeleza na kukuza biashara yao kwa kujifunza mbinu mpya za kibiashara, kupata wabia na masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi.