Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Viwango Barani Afrika (ARSO) utakaofanyika kuanzia Juni 23 hadi 27, 2025, katika visiwa vya Zanzibar,


Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Viwango Barani Afrika (ARSO) utakaofanyika kuanzia Juni 23 hadi 27, 2025, katika visiwa vya Zanzibar, ambapo Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Akizungumza leo Mei 27, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Ashura Katunzi, amesema mkutano huo unatarajiwa kuwahusisha takribani wageni 300 kutoka zaidi ya nchi 50, wakiwemo wanachama wa ARSO na wadau wa viwango kutoka ndani na nje ya Afrika.

Dkt. Katunzi amesema kuwa tukio hili litakuwa fursa ya kipekee kwa Tanzania kutangaza bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, hususan kwa wazalishaji wanaotafuta masoko ya nje ya nchi, hivyo , ametoa wito kwa wazalishaji na watoa huduma wa ndani kushiriki na kudhamini, ili kutangaza bidhaa na huduma zao kwa wageni wa kimataifa.