Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania na Rotterdem kushirikiana katika tafiti zakuondoa umaskini nchini


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Sempeho Manongi amekutana na kuzungumza na ujumbe kutoka Taasisi ya Kituo cha Kimataifa cha Masomo ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Erasmus cha Rotterdem Nchini Uholanzi  ulioongozwa na Prof. Peter Knorringa Octoba 06,2023 katika Ofisi Za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma.


Katika mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya Taasisi hiyo inayoshiikiana na Taasisi ya Utafiti wa
Kupunguza umasikini Tanzania (REPOA) na Serikali katika kuwajengea uwezo Watumishi wa Serikali, Taasisi za Elimu, Utafiti na Sekta Binafsi ili kuongeza
ufanisi katika utendaji kazi na kutafuta masoko.