Habari
Tanzania na Uturuki waimarisha uhusiano wa biashara

Tanzania na Uturuki waimarisha uhusiano wa biashara
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Ashatu Kijaji (Mb.) alisema Tanzania na Uturuki zimeendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi kubwa ambapo wafanyabiashara baina ya mataifa hayo wamekuwa wakifanya biashara yenye thamani kubwa katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa miundombinu
Waziri Kijaji aliyasema hayo Septemba 19, 2023 akiwa na Balozi wa Uturuki nchini, Dk. Mehmet Gulluoglu walipofungua Mkutano wa Biashara (B2B) kati ya Tanzania na Uturuki uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa biashara kati ya nchi hizo mbili.
Aidha, alitoa wito kwa wafanyabiashara wa kitanzania walioshiriki Mkutano ambao utaongeza chachu ya biashara kwa kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye baina ya mataifa hayo mawili katika kukuza na kuendeleza biashara zao na kujipima baada ya miezi sita (6) kuwa bidhaa ngapi zimeuzwa na ngapi zimepokelewa kutoka uturuki
Aidha, Waziri Kijaji alibainisha kuwa mauzo ya bidhaa kutoka Uturuki kwenda Tanzania yameongezeka kwa kiwango cha wastani cha asilimia 17.3 katika kipindi cha miaka 26 iliyopita kutoka Dola za Marekani milioni 4.55 mwaka 1995 na kufikia Dola za Marekani milioni 500 mwaka 2022
Vilevile alibainisha kuwa mwaka 2021, Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 37.6 nchini Uturuki na bidhaa kubwa ilikuwa dhahabu ambayo ilikuwa Dola milioni 14.9 na tumbaku ghafi Dola za Marekani milioni 11.2.
Naye Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu alisema wafanyabiashara kutoka kampuni 30 za uturuki katika sekta mbalimbali zikiwemo teknolojia, ujenzi na utengenezaji wa nguo zimekuja kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji na ubia na wawekezaji watanzania wanaowakilishwa na kampuni 100.
“Tanzania na Utururi hatushindani kibiashara bali ni washirika ambao tumekuwa tukisaidiana kwenye kuimarisha biashara mbalimbali kwa watanzania kupeleka bidhaa uturuki na Uturuki kuleta bidhaa hapa Tanzania,”