Habari
Tanzania na Zambia zakubaliana kutatua changamoto za kibiashara

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia Bi Lillian Bwalya wakitia saini Makubaliano ya kutatua changamoto za kibiashara 8 kati 24 kati ya Tanzania na Zambia wakati wa Mkutano wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika 09 - 10/10/2023 katika Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani- Tunduma, Songwe. Changamoto 16 zitatatuliwa kabla ya Disemba 2023.