Habari
Tanzania ni salama kwa ufanyaji biashara na uwekezaji Afrika

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb. Ametoa wito kwa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza nchini kwa kuwa hali ya uwekezaji na mazingira ya ufanyaji biashara ni salama.
Kigahe ameyasema hayo Oktoba 4, 2023 wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Wazalishaji wa Tanzania (TIMEXPO) yanayofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Aidha, Kigahe amesema Serikali inahakikisha mazingira ya uwekezaji ni rafiki na hivyo waje kwa wingi kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini Amesema hata mazingira ya ufanyaji biashara bado ni rafiki na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuichagua Tanzania katika biashara zao.
Maonesho ya kimataifa ya wazalishaji wa viwanda Tanzania (TIMEXPO) yanafanyika kwa siku tatu na yanashirikisha wazalishaji wa ndani na nje ya nchi.