Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

TANZANIA YANG'ARA UZINDUZI WA WIKI YA PROGRAMU YA UTALII, EXPO 2025 OSAKA.


TANZANIA YANG'ARA UZINDUZI WA WIKI YA PROGRAMU YA UTALII, EXPO 2025 OSAKA.

Naibu Kamishna wa Expo ambaye pia ni Balozi wa Tanzania Nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda, kwa niaba ya Bi.Latifa Khamis, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade na Kamishna wa Expo jana alizindua programu ya kutangaza Biashara za Utalii kwenye Maonesho ya Dunia Expo 2025 Osaka. Akielezea programu hiyo amesisitiza wadau wa Utalii kuitumia vizuri wiki hii kwa kufanya mikutano na wadau ili kutangaza Utalii na uwekezaji wake Tanzania.

Naye Mratibu wa Banda la Tanzania, Bw. Deo Shayo amelezea kuwa TanTrade kama mratibu inashirikiana na Wadau wa sekta za umma na binafsi kuratibu programu tofauti nane (8) ambazo zitafanyika ndani ya miezi sita ya Expo ambapo moja wapo ni hiyo ya utalii.

Aidha, Eneo la Tanzania limetembelewa na Mwenyenyikiti wa Sekta binafsi Bi.Angelina Ngalula ambaye ametoa pongezi kwa Tanzania kushiriki na kuahidi kuendelea kuhamasisha ushiriki wa Sekta binafsi hasa kwenye kongamano la biashara ili kuwa na tija zaidi.

 

 
 
  •