Habari
TANZANIA KUFIKIA UCHUMI WA DOLA TRILIONI MOJA KWA KULINDA VIWANDA VYA NDANI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imesema ili kufikia lengo la Taifa la uchumi wa Dola Trilioni 1 ni muhimu kuhakikisha Serikali inalinda viwanda vya ndani kwa ajili ya kuzalisha, kuajiri, kupata fedha za kigeni ili kuhakikisha uchumi na ustawi za Tanzania ukua.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb), wakati akizungumza mara baada ya kutembelea Viwanda vya Yogi Polypack Ltd, Neelkath Chemicals Ltd na Tanga Cement PLC Jijini Tanga Aprili 12, 2026 kwa lengo la kuona shughuli za uzalishaji pamoja na changamoto zake.
Amesema Kamati hiyo inachukua changamoto za wamiliki wa Viwanda na kuziwasilisha katika ngazi husika ili ziweze kupatiwa utatuzi.
