Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WANAWAKE NI NGUZO MUHIMU YA UKUAJI WA BIASHARA NA UCHUMUMI


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amebainisha kuwa maono ya Taifa kwa miaka 25 ijayo yanalenga kukuza uchumi kwa kiwango kikubwa, ambapo asilimia 70 ya utekelezaji wake unategemea mchango wa sekta binafsi.

Amesisitiza kuwa wanawake ni nguzo muhimu iliyo katikati ya ukuaji huo, hivyo Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wanawake na vijana kuchangamkia fursa za kiviwanda na kibiashara ili kuwa sehemu ya safari ya maendeleo ya kiuchumi nchini.