Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania yashiriki  Mkutano wa SCTIFI ngazi ya Makatibu wa Wakuu wa EAC


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundu akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Makatibu Wakuu wa kilichofanyika jijini Arusha tarehe 08 Februari 2024.

Mkutano huo ulijumuisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi , Congo DRC na Sudani uliongozwa na  Südani Kusini  kama Mwenyekiti na utafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Mawaziri utakaofanyika Februari 9, 2024 jijini Arusha.

Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka ya Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi.