Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania yawaonyesha Wageni Fursa mbalimbali za  Uwekezaji 


 

 

Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja (Mb.) amewahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa  kuna fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo Maliasilili na Utalii, Kilimo, Madini, na utalii wa fukwe.  

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa jukwaa la Uwekezaji lilifanyaka tarehe 22 Octoba, 2022 katika  katika Ukumbi wa Mlimani City Jijijni Dar es salaam.

Aidha, Waziri Masanja amesema jukwaa hilo hufanyika sambamba na maonesho ya utalii yanayojumuisha nchi 20 kutoka mataifa mbalimbali duniani, alisisitiza jukwaa hilo limelenga kuwataarifu wageni kujifunza fursa mbalimbali uwekezaji Tanzania. 

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara nchini ikiwemo kuanzisha mfumo wa dirisha moja la huduma kwa wawekezaji ili kurahisisha huduma ya usajili upatikanaji vibali kwa wakati mmoja  

Aidha, aliongeza kuwa Serikali inatarajia kupeleka mapendekezo ya Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022 Bungeni yenye lengo la kuboresha mazingira ya Uwekezaji katika sekta zote za kiuchumi nchini.