Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Ujumbe wa Tanzania kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uchukuzi, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Sultan ya Oman


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda ma Biashara Dkt.Hashil T. Abdallah akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) ameongoza Ujumbe wa Tanzania kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uchukuzi, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Sultan ya Oman Mhe.Said Al Mawali Aprili 28,2025 katika Hoteli ya St.Regis Jijini Muscat-Oman.

Mazungumzo hayo yamelenga kujadili mambo mbalimbali mbali na ushirikiano wa kidiplomasia pia Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano na Oman katika sekta ya posta na biashara ya mtandaoni (E-commerce), kuharakishwa kwa utekelezaji wa Mkataba wa Huduma za Anga (BASA) uliosainiwa Juni 2024 ambao utaruhusu Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) liruhusiwe kuanzisha safari za moja kwa moja kwenda Muscat, Oman, ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa pamoja na kuanzishwa kwa meli maalum ya mizigo kati ya Oman na Tanzania kutokana na mahitaji makubwa ya uagizaji wa wanyama hai, matunda, na viungo.

Vilevile Serikali ya Tanzania imefurahishwa na kukamilika kwa upembuzi kwa ajili ya kuanzisha kituo cha miundombinu ya usafirishaji na kuanza kuona makubaliano haya kwa vitendo ambayo yanatarajiwa kuanza mwaka 2025 hadi 2045.

Pamoja na hayo Serikali ya Tanzania imewakaribisha wawekezaji kutoka Nchini Oman kuangalia fursa zilizopo nchini, ikitaja mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji yaliyoimarishwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha mazungumzo hayo pia yqmehudhuriwa na Balozi wa Tanzania Nchini Oman Mhe.Fatma Abdallah,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Nchini Tanzania DktStephen Nindi, Viongozi wa sekta binafsi na Maafisa kutoka Wizara hizo.