Habari
TARATIBU ZA URASIMISHAJI WA BIASHARA KWA KUSAJILI NA KUTOA LESENI ZA BIASHARA NA VIWANDA KWA NJIA YA MTANDAO KUPITIA BRELA ZIMESAIDIA KUVUTIA WAWEKEZAJI
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ameeleza kuwa taratibu za urasimishaji wa biashara nchini kwa kusajili na kutoa Leseni za biashara na viwanda kwa njia ya mtandao kupitia BRELA zimesaidia kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuwezesha nchi kuwa katika kiwango bora cha ufanyaji biashara duniani.
Mhe. Kigahe ameeleza hayo Novemba 08, 2021 katika kikao cha mafunzo kwa Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania kuhusu makapuni na majina ya biashara; leseni za biashara na za viwanda; na miliki ya ubunifu yaliyotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) katika ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma.
Mhe. Kigahe amebainisha kuwa utoaji huduma za BRELA kwa njia ya mtandao umepunguza sana na kudhibiti vishoka waliowasumbua wateja wakati walipohitaji huduma kama kusajili makampuni na majina ya biashara.
Aidha, Mhe. Kigahe ameeleza kuwa kupitia utekeleza wa Blueprint watapitia baadhi ada na tozo zinazotozwa na BRELA kwa kuziondoa au kuzipunguza ili Watanzania waweze kurasimisha biashara zao vilevile baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba wateja kwenye mtandao zimetatuliwa na wanaendelea kufanyia maboresho Zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni BRELA, Bw. Andrew Mkapa wakati akitoa mafunzo juu ya usajili wa makampuni na majina ya biashara amefafanua kuwa baadhi ya wateja wamekuwa wakishidwa kutofautisha kati ya kampuni na jina la biashara huku akieleza kisheria ni vitu viwili tofauti.