Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

TEMDO shirikianeni na Taasisi nyingine kuwawezesha wananchi kuanzisha viwanda vidogo vidogo


Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Leo Mei 28, 2022 ameitaka Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) kufanya kazi kwa ushirikiano na Taasisi nyingine katika kutumia mifuko 62 ya uwekezaji kuwawezesha wananchi kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji sukari kwa kutumia mitambo inayozalishwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kuongeza ajira na kuondoa upungufu wa sukari nchini.