Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SEKTA YA UBASHIRI YACHANGIA BILIONI 260 PATO LA TAIFA


Serikali imebainisha kuwa sekta ya ubashiri imekuwa muhimili muhimu wa kiuchumi nchini ikichangia takriban TZS bilioni 260 kama kodi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kupitia kampuni 62 zilizopewa leseni.

Hayo yamebainishwa Aprili 30, 2026 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo wakati akizindua Kampuni mpya ya ubashiri ya Vunjabei Bet, iliyo chini ya Mkurugenzi Mkuu, Bw. Fred Ngajiro (Vunjabei).

Bw. Mbwasi amesema uwekezaji huo utaongeza Pato la Taifa, utakuza michezo, utatoa ajira, utavuatia uwekezaji nchini na kukuza uchumi wa kidigitali.

Katika hatua nyingine, Bw. Mbwasi ameiagiza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na taasisi nyingine kama BRELA na SIDO kuhakikisha zinawatambua na kuwasaidia wafanyabiashara wazawa wanaojituma ili kampuni zao ziweze kujisimamia na kukua zaidi.

Pia, ametoa rai kwa kampuni ya Vunjabei Bet na sekta nzima ya ubashiri kuzingatia sheria, kulipa kodi kwa wakati na kuhamasisha ubashiri wa na wenye uwajibikaji ili kulinda jamii.