Habari
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amekutana na ujumbe kutoka China
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amekutana na ujumbe kutoka China na kufanya kikao kilichoangazia maswala mbalimbali ya kibiashara, teknolojia na fursa kwa bidhaa zenye tija kama vile kahawa, mvinyo, mwani, samaki, maparachichi simenti na madini Aprili 27, 2025 jijini Dar es Salaam.
Naibu Kigahe ametumia fursa hiyo kuukaribisha Ujumbe huo kutoka China kuja kuwekeza kwenye sekta ya viwanda na tekinolojia.
Aidha, Ujumbe huo umelenga kuimarisha maendeleo ya viwanda kwa lengo na kuongeza thamani kwenye bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania huku, wakiadhimia kuleta wataalamu wa kutambua bidhaa zenye tija kwenye soko la China hali itakayoongeza asilimia ya bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kwenda China.