Habari
Wizara imepongeza utendaji wa watumishi kwa kufanya kazi kwa weledi.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mhe. Mariam Ditopile kwaniaba ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika ,
imepongeza utendaji wa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kufanya kazi kwa weledi.
Pongezi hizo zimetolewa Mei 13, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati wa semina kwa wabunge wa kamati hiyo.
Mhe. Ditopile amesema kuwa, semina ilikuwa na manufaa makubwa kwa jamii ili ilikuwa na mada inayohusiana na madhara ya matumizi ya pombe, vipimo vya bidhaa mbalimbali na umuhimu wa mapato.
Mhe.Ditopile ameongeza kuwa walikuwa na majadiliano mazuri na wizara pamoja na taasisi husika, ambapo wamepata uelewa mpana kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hizo.
“Wajumbe wamepata uelewa kuhusu mifumo ya kutambua bidhaa zinazozalishwa nchini ili kubaini uhalali wake, jambo ambalo litasaidia katika kuongeza makusanyo ya mapato,” alisema Ditopile, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum.
Mbunge huyo alisisitiza kuwa TBS na WMA zihakikishe waingizaji wa bidhaa nchini wanafuata vigezo vilivyowekwa ili mlaji wa mwisho apate bidhaa salama na zenye ubora.