Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WIZARA ya Viwanda na Biashara imeomba kuidhinishiwa na Bunge kiasi cha sh. Bilioni 135.7 kwa ajili ya utekelezaji majukumu yake.


 

 

WIZARA ya Viwanda na Biashara imeomba kuidhinishiwa na Bunge kiasi cha sh. Bilioni 135.7 kwa ajili ya utekelezaji majukumu yake.

Hayo yamesemwa bungeni Dodoma leo na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Selemani Jafo, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Jafo amesema kati ya fedha hizo, sh. Bilioni 93.9 ni matumizi ya kawaida, na sh. Bilioni 41.8 ni matumizi ya Maendeleo.

Waziri huyo amesema katika sh. Bilioni 93.9 za matumizi ya kawaida, sh. Bilioni 75.8 ni Mishahara na sh. Bilioni 18 ni matumizi mengineyo.

Aidha, amesema kati ya sh. Bilioni 41.8 zinazoombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, sh. Bilioni 27.8 ni fedha za ndani na sh. Bilioni 14 ni fedha za nje.