SEKTA YA BIASHARA YA UTALII KIVUTIO EXPO OSAKA 2025
Katika Maonesho ya Expo Osaka 2025, Tanzania imeonekana zaidi kuvutia kwenye eneo la Utalii ambapo idadi kubwa ya watembeleaji wameendelea kuingia kwenye Banda kupata maelezo ya Mlima Kilimanjaro, Mbuga za Wanyama, Fukwe za Zanzibar, pamoja na bidhaa mbalimbali ikiwemo Chai, kahawa na Karafuu. Akitoa tathmini ya uratibu kwa Wageni wanaotembelea, Meneja wa Banda la Tanzania kutoka TanTrade Bw. Deo Shayo amesema _"Wiki hii TanTrade imeweka program za Utalii ikiwa ni miongoni mwa program nyingi za EXPO ambapo tumewaratibu wadau wetu wa Biashara ya utalii wakiwemo Ngorongoro, TANAPA, TAWA na Bodi ya Utalii TTB ili watangaze vivutio vya Utalii Tanzania. Kwa kweli mwitikio wa watembeleaji ni Mkubwa"
Aidha, Bw. Shayo alisistiza "Watembeleaji wengi wanaonekana kupenda zaidi mlima Kilimanjaro, Serengeti na Utalii wa Fukwe Zanzibar. Kinacholeta hamasa ni mhuri wanaogonga kwenye Banda wa chapa Kilimanjaro ambapo hadi kufikia tarehe 27 Aprili 2025 umeshavutia watazamaji (likes) wa mataifa mbalimbali zaidi ya 5,000".
Baada ya kukamilisha programu ya Utalii tarehe 6 Mei 2025, TanTrade chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda - Zanzibar itaendelea kuratibu programu nyingine Saba zinazotegemewa hadi kufikia Oktoba 2025.