Habari
USHIRIKISHWAJI WANAWAKE NA VIJANA NI KICHOCHEO CHA BIASHARA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman amesema ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika ngazi mbalimbali ikiwemo nafasi za uwakilishi ni hatua moja wapo muhimu itakayochochea ufanisi katika biashara zinazoendeshwa na kundi hilo barani Afrika.
Ameyasema hayo Septemba 14, 2022 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi wakati akifunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika ulioanza Septemba12 hadi 14, 2022.
Kauli mbiu ya mkutano huu ilikuwa ni Wanawake na Vijana: Injini ya Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika. Hii ni kauli mbiu nzuri kabisa na ninaomba kuwashukuru na kuwapongeza wote walioshiriki katika kuibuni na kuipendekeza,"amesema.
"Nina imani kwamba, katika siku zote tatu mlizokuwepo hapa, mtakuwa mmeanza kuitekeleza kauli mbiu hii bila ya shaka. Hii ni kauli mbiu inayoishi na kama tukiendelea kuitekeleza kwa vitendo tutaona wanawake na vijana wengi zaidi wakishiriki na kunufaika katika biashara na hivyo kupelekea uchumi wetu kuzidi kukua na kuimarika, ikiwa ni pamoja na ajira.
"Wito wangu kwetu sote ni kwamba tuendelee kuitekeleza kauli mbiu hii kwa vitendo hata baada ya mkutano huu, kwani ni dira muhimu sana kwa wanawake na vijana wetu kote barani Afrika,"amesema Mheshimiwa Othman kwa niaba ya Rais Dkt.Mwinyi.
Pia amesema,anatarajia maazimio yote yaliyofikiwa katika mijadala ni msingi na chachu ya ushiriki wa wanawake na vijana wengi zaidi katika shughuli mbalimbali za biashara barani Afrika na duniani kwa ujumla na yatafanyiwa kazi na Sekretarieti ya AfCFTA kwa kushirikiana na nchi wanachama.
"Itifaki hii inatarajiwa kusaidia kuimarisha uwezo wa wanawake na vijana katika kutumia fursa zinazotokana na Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika. Kwa hivyo, natumia nafasi hii kuwaomba wanawake na vijana wa Afrika kuhakikisha kwamba mnatumia vyema fursa zinazopatikana katika Bara la Afrika na kwa manufaa ya nchi zetu za Afrika kwa kuzingatia utajiri tulio nao,"amesema.
Makamu wa Rais wa Kwanza alitumia nafasi hiyo kuzipongeza na kuzishukuru nchi zote za Afrika kupitia Sekreterieti ya Eneo Huru la Biashara la Afrika, kwa heshima kubwa waliyoipatia Tanzania