Habari
Uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II)
Uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli azindua Awamu ya pili ya Programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo (ASDP II) katika ukumbi wa Mwalimu J.K Nyerere jijini Dar es salaam tarehe 4 Juni, 2018. Katika hotuba yake Rais Magufuli amesema kuwa atahakikisha pesa yote itakayotolewa na wadau wa maendeleo katika mradi huu zitatumika vizuri na hakuna hata senti moja itakayopotea, baada ya uzinduzi huo Rais alikabidhi vitabu vya utekelezaji wa mradi huo wa kuendeleza sekta ya kilimo kwa Wizara za kisekta ikiwemo Wizara ya Viwanda ambao ndio watekelezaji wakuu wa mradi huu. Waziri wa Kilimo Mhe. Mhandisi Dkt. Charles Tizeba (Mb) amesema kuwa program hii awamu ya kwanza imesaidia kuongeza uzalishaji na nchio kujitosheleza kwa chakula kwa wastani wa asilimia 123 ambao unazidi mahitaji ya chakula katika nchi ambayo ni asilimia 100.